Tazama picha za matukio mbalimbali yaliyojiri bungeni leo May 16, 2018 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 17, 2018

Tazama picha za matukio mbalimbali yaliyojiri bungeni leo May 16, 2018


Kikao cha 30, mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea Bungeni mjini Dodoma muda huu, likiwa limeongozwa na Mwenyekiti wa Bunge, Azzan Zungu,ambapo kipindi cha maswali na majibu kimeendelea; Tazama matukio katika picha
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Madaba, Mheshimiwa Joseph Mhagama kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 16, 2018
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi ,Vijana Ajira, na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiteta na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, Bungeni jijini Dodoma, Mei 16, 2018
Waziri wa Kilimo na Mifugo, Luhaga Mpinda akitoa maelezo kuhusu uhakika wa usalama wa nyama wanayokula watanzania, Bungeni jijini Dodoma, Mei 16, 2018
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akizungumza na wanawake kutoka Mbeya waliotembelea Bunge kwa mwaliko wa Naibu Waziri wa Kilimo Mary Mwanjelwa kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 16, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. Kulia ni Mbunge wa Lupa, Bvictor Mwambalaswa na watano kulia ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinda
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma, Mei 16, 2018.

Loading...

No comments: