TCRA watoa leseni kwa Blogs na Online TV, waeleza sababu kuu 3 za kufanya zoezi hilo (Video) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, May 26, 2018

TCRA watoa leseni kwa Blogs na Online TV, waeleza sababu kuu 3 za kufanya zoezi hilo (Video)

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekabidhi leseni za kufanya huduma ya kutoa habari kwa njia ya mtandao kwa Blogs, Online TV na Online Redio ambazo zimekamilisha usajili. Bongo5, Michuzi pamoja na Lemutuz ni moja kati ya Blogs na Online TV ambazo zimekabidhiwa leseni ya kufanya huduma hizo huku baadhi ya blogs kama Muungwana,Dar24, Millardayo, 8020 Fashion na Mwanaharakati Mzalendo na nyingine nyingi zikipewa leseni ya kurusha matangazo kupitia blogs pekee.
Akizungumza Ijumaa hii na waandishi wa habari na Wanablogs katika ukumbi wa TCRA, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba alisema zoezi hilo endelevu lina lengo la kuzuia uanzishwaji holela wa blogs na online tv ambao unaweza kusababisha madhara kwa jamii.
“Jambo la kwaza tunazuia uanzishwaji holela wa vyombo vya habari mtandaoni usiokidhi viwango vinavyotakiwa, ikumbukwe kwamba umiliki wa vyombo vya habari bila tozo unaweza ukaleta utitiri wa vyombo hivi na ikawa changamoto katika usimamizi na kwa jamii,” alisema Mhandisi James Kulaba.
Bongo5 Media Group imekabidhiwa leseni ya kufanya huduma ya habari kwa njia ya mtandao, kupitia Blogi ya bongo5.com pamoja na Online TV ya Bongo5. Katika picha ni Content Producer wa Bongo5, Yasini Ng’itu akipokea leseni hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba.
Aliongeza, “Jambo la pili ni kuleta ushindani sawa,itakuwa sio vyema vyombo vya habari vinavyotumia majukwaa mengine kulipia leseni wakati vyombo vya mtandaoni havilipii gharama yoyote. Na jambo la tatu ni kutambua watu wenye nia safi ya kutoa huduma hii ya maudhui mtandaoni kwa jamii yetu,”
Katibu wa Tanzania Blogers Network, Krantz Charles Mwantepele ambaye pia ni mkurugenzi wa Mwanaharakati Mzalendo Blog akikabidhiwa leseni yake na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba.
Mhandisi James amezitaka online tv pamoja na blogs mbalimbali kuendelea kujitokeza ili waweze kujisajili na kufanya kazi kwa uhuru huku akidai hatua hiyo itafungua milango ya kibiashara kwa blog na online tv.CHANZO ;BONGO5 
Loading...

No comments: