Vodacom M-Pesa yasherehekea miaka kumi ya kubadilisha maisha ya Watanzania - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, May 29, 2018

Vodacom M-Pesa yasherehekea miaka kumi ya kubadilisha maisha ya Watanzania

MKurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania ,Ian Ferrao (katikati) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi  wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia   (kushoto)  wakati akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  jijini Dar es salaam,  wakati wa mkutano uliohusu maadhimisho ya sherehe za miaka 10 ya M-Pesa  yatakayofanyika juni 13 , 2018.


MKurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao (katikati)  akifafanua jambo kwa  waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, kuhusiana na maadhimisho ya sherehe  ya Miaka 10 ya M-Pesa yatakayofanyika juni 13 , 2018. wakati wa   mkutano  na waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi  wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia  na  Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya bidhaa na masoko wa M-pesa,Polycarp Ndekana.

MKurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao (katikati)  akifafanua jambo kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam jana, kuhusiana na maadhimisho ya sherehe  ya Miaka 10 ya M-Pesa itakayofanyika Juni 13, 2018, wakati wa   mkutano  na waandishi  uliofanyika makao makuu ya Kampumi hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi  wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia.  


MKurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania ,Ian Ferrao (katikati) akifafanua jambo kwa  waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, kuhusiana na maadhimisho ya sherehe  ya Miaka 10 ya M-Pesa yatakayofanyika juni 13 , 2018. wakati wa   mkutano  na waandishi  uliofanyika makao makuu ya Kampumi hiyo  Vodacom Tower Morocco jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi  waMawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia   na  Mkuu wa kitengo cha maenendeleo ya bidhaa na masoko wa M-pesa, Polycarp Ndekana.

MKurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania ,Ian Ferrao (katikati) akifafanua jambo kwa  waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, kuhusiana na maadhimisho ya sherehe  ya Miaka 10 ya M-Pesa yatakayofanyika juni 13 , 2018. wakati wa   mkutano  na waandishi  uliofanyika makao makuu ya Kampumi hiyo  Vodacom Tower Morocco jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi  waMawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia   na  Mkuu wa kitengo cha maenendeleo ya bidhaa na masoko wa M-pesa, Polycarp Ndekana.

 Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye mkutanao wa  Vodacom Tanzania Plc, uliohusu  maadhimisho ya kusherehekea  Miaka 10 ya M-Pesa yatakayofanyika Juni 13 , 2018.  uliofanyika makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

MKurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao (kulia)  akifafanua jambo kwa  waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maadhimisho ya sherehe  ya Miaka 10 ya M-Pesa yatakayofanyika Juni 13 , 2018. wakati wa   mkutano  na waandishi wa habari  uliofanyika makao makuu ya Kampuni hiyo  Vodacom Tower Morocco jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi  wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia   na  Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya bidhaa na masoko wa M-pesa, Polycarp Ndekana.

Vodacom M-Pesa yasherehekea miaka kumi ya kubadilisha maisha ya Watanzania
Dar es Salaam, May 29, 2018 – Vodacom Tanzania PLC leo imetimiza miaka kumi tangu kuzinduliwa kwa huduma ya M-Pesa. Kwa miaka hiyo kumi, Vodacom M-Pesa imejikita kwenye kutoa huduma mbali mbali kama kulipia huduma na bidhaa, huduma za kibenki, kuweka na kukopa pesa, kutuma pesa nje ya nchi na huduma nyingine nyingi. Huduma hizo zote zinapatikana kwa njia rahisi sana ya huduma ya pesa kwa njia ya mtandao ambayo ilikuwepo tangu mwanzoni.
Leo hii, Vodacom M-Pesa inaongoza Tanzania kwa huduma za kifedha za mtandao kwa makampuni ya simu za mkononi kwa asilimia 42 huku ikiwa na watumiaji hai 8.2 milioni, mawakala 106,000, wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 2,000 wafanyabiashara wadogo 15,000 na benki 30 ambao zimeunganisha kwenye mtandao wa Vodacom M-Pesa. Kwa mtandao mpana na imara, M-Pesa imeweza kutoa huduma kwa Watanzania vijijini na mijini ambapo wameweza kutumia huduma halali ya kifedha na kusababisha kukua kwa uchumi wa Taifa kutoka 58% 2013 na 44% 2009 hadi 65% kwa mwaka 2017,.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Ian Ferrao alisema, M-Pesa imezalisha ajira za moja kwa moja na ambao si za moja kwa moja zaidi ya 200,000- wengi wao wakiwa ndio wanaanza ujasiriamali – na kufanya zaidi ya Tzs 617 bilioni kulipwa kama kamisheni kwa mawakala kila mahali Tanzania. Zaidi ya Tzs 120 bilioni zimetolewa kama mikopo tangu kuzinduliwa kwa M-Pawa (huduma ya kuweka na kukopa) mwaka 2014 na hivyo kufanya Wajasiriamali kuanzisha biashara mpya na hivyo kubadilisha hali ya maisha yao ya kila siku. Mpaka sasa zaidi ya Tzs 99 bilioni zimetolewa kama faida kwa watumiaji wa M-Pesa milioni 8 na zaidi ya Tzs 355 bilioni zimewekezwa kwenye benki mbali mbali hapa Tanzania. Hii inaamanisha kuwa pesa yako haikai bure ndani ya account ya M-Pesa, pesa yako inaendelea kutengeneza faida kupitia kwenye akaunti yako kwa muda wote inapokaa humo.
Mafanikio ya M-Pesa kwa miaka kumi iliyopita yanamaanisha mwanzo mpya wa malipo kwa njia ya kidijitali hapa Tanzania. M-Pesa imegusa na kubadilisha maisha ya mamilioni ya Watanzania pekee. Miaka kumi iliyopita, M-Pesa ilimaanisha kutuma na kupokea pesa kutoka kwa mteja mmoja kwenda kwa mwingine. Leo hii, M-Pesa inaamanisha maisha ya kila siku na inaendelea kukua kwa huduma mbali mbali. Vodacom M-Pesa ndio mtandao pekee hapa Tanzania wenye kutumia huduma za QR code na hivyo kuongoza kwenye huduma za ziada na nafuu na kuwa teknolojia inayoongoza kiuwekezaji na sio Tanzania tu bali barani Afrika,” alisema Ferrao.

1
Ian alipongeza juhudi za Vodacom kuboresha na kukuza huduma ya fedha kwa simu za mkononi hapa Tanzania na kuchangia kukuza uchumi wa Tanzania kwa kutengeneza ajira, kukuza biashara na sana sana wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na kukuza uchumi wa nchi. Leo zaidi ya asilimia 35 ya uchumi wa nchi (GDP) unachangiwa kwa kupitia M-Pesa huku kila mwezi zaidi ya miamala yenye thamani ya sh 1.2 trilioni ikifanyika.
Kusherekea miaka kumi ya mafanikio ya Vodacom M-Pesa kunakuja baada ya kuzawadiwa zawadi ya GSMA Mobile certification kwa usalama na utaalam uliotukuka na kuifanya Vodacom M-Pesa mojawapo ya bidhaa za kampuni ya simu ya mkononi kupata cheti cha kimataifa.
Ian Ferrao aliongeza kuwa maadhimisho ya kutimiza miaka kumi yatafanyika mikoa mbali mbali hapa Tanzania ikiwa ni kuonesha shukrani kwa wafanyakazi, mawakala wa M-Pesa na wafanyabiashara ambao kwa pamoja wameweza kuchangia safari hii ya mafanikio.
Lakini mbali na mafanikio hayo, sisi Vodacom tunaamini ndio kwanza ndio tumeanza. Lengo letu ni kuwa kampuni inayoongoza kidijitali hapa Tanzania na kuendelea kuifanya M-Pesa kuwa ya kidijitali zaidi. Huu ni mwanzo wa mafanikio ambapo tunaifanya M-Pesa kuwa na ubunifu zaidi. Naiona Tanzania ambayo kila kitu anachotaka mteja kinaweza kupatikana kupitia zana ya M-Pesa ambapo wateja wanaweza kulipia huduma na bidhaa ndani ya nchi na nje ya nchi kama China, Amerika na zaidi,” aliongeza.
Tunatoa shukrani kwa wafanyakazi, wateja, washirika wetu, wadhiti wakiwepo BoT na TCRA na wale wengine wote waliochangia safari yetu ya mafanikio. M-Pesa inaendelea kuwa nguzo imara kwa Vodacom Tanzania. Tumedharia kufanya malipo kwa njia ya kidijitali hapa Tanzania,” aliongeza Ferrao.
Loading...

No comments: