Watu 45 wamevuta hewa yenye sumu Dar es salaam - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, May 23, 2018

Watu 45 wamevuta hewa yenye sumu Dar es salaam

Watu 45 wameathirika baada ya kuvuta hewa yenye sumu kutoka kiwanda cha kutengeneza sabuni cha ROYAL kilichopo Mabibo external Jijini Dar es Salaam.


Akitibitisha kutoka kwa tukio hilo, Mkuu wa wilaya ya Ubungo  Bw. Kisare  Makori amesema tatizo hilo limetokea baada ya kuwepo kwa hitilafu katika moja ya mtambo wa kuchuja tindikali lakini mpaka sasa, wamiliki wa kiwanda hicho wameshadhibiti na zoezi la uzalishaji linaendelea kama kawaida.

"Kuna watu watatu ambao walipata madhara zaidi yaani walikuwa wanatapika na kuumwa vichwa lakini wameshapatiwa matibabu na wengine 42 walienda katika kituo cha afya kupatiwa huduma kutokana na kuhisi kuathirika na hewa hiyo waliyoivuta wakati wakiwa kiwandani", amesema Makori. 
Loading...

No comments: