Wazazi Waliomshtaki Mtoto Wao kwa Kugoma Kuondoka Nyumbani Washinda Kesi Jaji Aamuru Aondoke - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, May 25, 2018

Wazazi Waliomshtaki Mtoto Wao kwa Kugoma Kuondoka Nyumbani Washinda Kesi Jaji Aamuru Aondoke


Wazazi Waliomshtaki Mtoto Wao kwa Kugoma Kuondoka Nyumbani Washinda Kesi Jaji Aamuru Aondoke
Wazazi wawili mjini New York wameshinda kesi waliyokuwa wakipambana kumuondoa kijana wao mwenye umri wa miaka 30 baada ya kukaidi kuondoka

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo katika mahakama ya juu ya jimboni humo, Jaji aliamuru kijana huyo aondoke nyumbani kwa wazazi wake.

Jaji Donald Greenwood alimwambia kijana huyo kuendelea kubaki nyumbani kwa miezi sita zaidi kama alivyoomba ''haikubaliki''

kijana Michael Rotondo ambaye alijiwakilisha mwenyewe mahakamani, amesema ''Sijui kwa nini hwawezi kusubiri kidogo kabla ya mimi kuondoka,Bwana Rotondo alieleza huku wazazi wakiwa wamekaa karibu na mwanasheria wao wakimtazama.

Alisema kuwa miezi sita ndio muda uli sawa kwa mtu ambaye alikuwa akiwategemea watu .

Jaji akiwa anatabasamu alimtaka kijana huyo azungumze na wazazi wake,na kuamua kwa hiyari kuondoka nyumbani, lakini Rotondo alikataa.

''Nataka uondoke hapo nyumbani'' Jaji Greenwood aliamuru, kwa mujibu wa kituo cha habari cha ABC

Instagram 'ni hatari zaidi kwa afya ya vijana'
Walipokuwa wakifungua mashtaka juma lililopita,Christina and Mark Rotondo walionyesha nakala ya nyaraka walizokuwa wakimuamuru kuondoka nyumbani tangu tarehe 2 mwezi Februari mwaka 2018.

Sehemu ya nakala zikiwa zimeandikwa ''Kuna kazi zinapatikana hata kwa wale wenye historia mbaya ya kufanya kazi kama wewe'' ''Nenda katafute kazi-unapaswa kufanya kazi!''
Loading...

No comments: