Zanzibar: Watu 9 wadakwa kwa kula hovyo mchana wakati wa Ramadhani - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, May 25, 2018

Zanzibar: Watu 9 wadakwa kwa kula hovyo mchana wakati wa Ramadhani

WATU tisa wamekamatwa kisiwani Zanzibar pamoja na Bar tatu kufungwa kwa makosa mawili tofauti tangu kuanza mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Katika kosa la kwanza, watu tisa wamekamatwa kwa kula chakula mchana katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani.

Aidha, katika kosa lingine Bar tatu zimefungwa kutokana na kuuza chakula mchana katika mkoa wa mjini Magharib Unguja hadi kumalizika kwa mwezi wa Ramadhani.

Mkuu wa mkoa huo, Ayoub Mohammed Mahmoud aliziagiza manispaa zote kusitisha leseni ya biashara za vileo katika kipindi chote cha mwenzi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema hatua hiyo itaimarisha imani za watu na kuzitaka manispaa hizo kusimamia agizo hilo na kufuata kanuni za wizara ya afya ili kuepusha mripuko wa maradhi.

“Ili waumini waweze kuukabili mwenzi huu lazima kwa wananchi kutumia fursa za Ramadhani kwa kufanya mambo mema ili Allah azikubalie swaumu zetu”alisema Ayoub..

Aidha, aliwataka watembeza watalii kutoa mwongozo kwa wageni kwa kufuata utaratibu ulio sahihi kwa kuvaa mavazi ya heshima na yanayo kubalika kutokana na mila,silka na utamaduni. 
Loading...

No comments: