ABDALLAH ULEGA AMEWATAKA WAJASIRIAMALI KUCHANGAMKIA FURSA YA UFUGAJI WA SAMAKI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, June 3, 2018

ABDALLAH ULEGA AMEWATAKA WAJASIRIAMALI KUCHANGAMKIA FURSA YA UFUGAJI WA SAMAKI

Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega na Mkurugenzi Mkuu wa TEDEF, Dokta Teresphory Kyaruzi 
Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka wajasiriamali nchini kuchangamkia fursa ya ufugaji wa samaki ili kukabiliana natatizo la uagiza samaki kutoka nje ya nchi, ambapo wengi wao wanakosa vigezo na ubora kwa walaji.
Waziri Ulega ameyasema hayo alipotembelea mradi wa ufugaji wa samaki wa Shirika la Kuinua Diplomasia ya Uchumi nchini (TEDEF), Ruvu Darajani mkoani Pwaniuliokabidhiwa kwa Kikundi cha Wahitimu wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini waliopewa jukumu la kusimamia mradi huo.
Katika mradi huo, waziri Ulega amejionea jinsi samaki aina ya sato na kambale wanavyofugwa na kuwataka wajasiriamali kuchangamkia fursa hiyo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega na Mkurugenzi Mkuu wa TEDEF, Dokta Teresphory Kyaruzi
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TEDEF, Dokta Teresphory Kyaruzi amemueleza naibu waziri changamoto mbalimbali zinawazowakabili.

https://youtu.be/2dBWqd3v0DY

Amos C Nyanduku
Loading...

No comments: