Antoine Griezmann, Paul Pogba waibeba Ufaransa dhidi ya Australia kombe la dunia

KOMBE LA DUNIA

Wachezaji Antoine Griezmann na Paul Pogba wamefanikiwa kuisaidia timu yao ya taifa ya Ufaransa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 1 dhidi ya Australia kwenye mchezo wa michuano ya kombe la dunia inayo endelea huko nchini Urusi.
Mchezo huo wa kundi C, umeshuhudia mshambuliaji wa taifa hilo,Antoine Griezmann akii yandikia Ufaransa bao la kwanza kwanjia ya mkwaju wa penati dakika ya 58 kisha Australia kuchomoa kupitia kwa mchezaji wake, Mile Jedinak kupitia njia hiyo hiyo ya adhabu ya penati kisha kiungo wa Ufaransa, Paul Pogba akihitimisha karamu ya mago dakika ya 80 na hivyo mchezo huo kumalizika kwa jumla ya mabao 2 – 1.
Mara baada ya ushindi huo timu ya Ufaransa inaongoza kwenye kundi C kwa kuwa na jumla ya alama 3 na mchezo mmoja, huku hapo baada Peru ikiikabili Denmark kwenye kundi hilo.
Kikosi cha Australia kina wachezaji, Ryan, Risdon, Milligan, Sainsbury, Behich, Jedinak, Mooy, Kruse, Leckie, Rogic, Nabbout.
Waliyotokea benchi, Degenek, Meredith, Cahill, Jurman, Luongo, Juric, Jones, MacLaren, Arzani, Vukovic, Petratos, Irvine.
Ufaransa kilikuwa na wachezaji, Lloris, Pavard, Varane, Umtiti, Hernandez, Kante, Pogba, Tolisso, Mbappe, Griezmann, Dembele.
Wakati wanao tokea benchi ni Kimpembe, Lemar, Giroud, Matuidi, Nzonzi, Mandanda, Rami, Fekir, Sidibe, Thauvin, Mendy, Areola.

Post a Comment

0 Comments