Brazil Yajiweka Pazuri kuelekea 16 bora Kombe la Dunia ....Ni Baada ya Kuichapa Costa Rica 2-0 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, June 23, 2018

Brazil Yajiweka Pazuri kuelekea 16 bora Kombe la Dunia ....Ni Baada ya Kuichapa Costa Rica 2-0


Mabao mawili yaliyofungwa na Philippe Countinho na Neymar Jr katika muda wa majeruhi yameipa Brazil ushindi wa 2-0 dhidi ya Costa Rica.

Countinho alifunga goli lake la pili katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi katika dakika ya ya kwanza ya nyongeza huku mwamuzi akikaribia kupuliza kipenga chake kuashiria kumalizika kwa mechi hiyo,

Neymar aliihakikishia Brazil ushindi kwa kupachika bao katika dakika ya saba ya nyongeza.

Mchezo huo ambao ulipigwa jana jioni, umempa nafasi Neymar Jr ya kufikisha mabao 56 ya kuifungia timu yake ya taifa na kumfanya sasa awe mchezaji wa 3 kufunga mabao mengi zaidi akitanguliwa na Ronaldo De Lima mwenye mabao 62 na Pele 77.

Kwa upande wa Coutinho bao la jana limekuwa la pili kwake kwenye Fainali za mwaka huu likitanguliwa na lile alilofunga kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Switzerland ambapo walitoka sare ya 1-1.
Loading...

No comments: