Diego Costa aipaisha Hispania.....Ni Baada ya Kuichapa bao 1-0 Iran - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 21, 2018

Diego Costa aipaisha Hispania.....Ni Baada ya Kuichapa bao 1-0 Iran


Hispania imefikisha pointi 4 baada ya ushindi wake wa kwanza wa bao 1-0 dhidi ya Iran jana na sasa inasubiri mechi yake ya mwisho dhidi ya Morocco.

Diego Costa ndiye aliyefunga bao pekee akigongeshewa mpira na beki wa Iran aliyekuwa akijaribu kuokoa.

Pointi 4 za Hispania zinawafanya kuwa na pointi sawa na Ureno na Iran inabaki kuwa na pointi zake 3.

Maana yake, kuvuka katika kundi timu tatu za Ureno, Hispania na Iran zina nafasi wakati Morocco tayari imefungashiwa virago.
Mechi za mwisho Ureno itakipiga na Iran huku Hispania ikicheza na Morocco ambayo tayari imeshaaga michuano hiyo. 
Iran ndio ipo kwenye wakati mgumu kwani inahitaji kushinda dhidi ya Ureno huku Ureno na Hispania zikihitaji ushindi au sare tu ili ziweze kutinga 16 bora.
Loading...

No comments: