Fernando Hierro arithi mikoba ya Lopetegui kuokoa jahazi la Hispania nchini Urusi - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 14, 2018

Fernando Hierro arithi mikoba ya Lopetegui kuokoa jahazi la Hispania nchini Urusi


Mkurugenzi wa michezo wa nchini Hispania,Fernando Hierro ametangazwa kurithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, ulen Lopetegui aliyetimuliwa hii leo siku ya Jumatano.
Hierro atakuwa kwenye majukumu mazito siku ya Ijumaa pale timu yake ya Hispania itakapo wakabili Ureno kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa kundi B.
Hispania yamtimua kocha wake, Julen Lopetegui siku moja kabla ya kombe la dunia
Nahodha huyo wazamani wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Real Madrid ataiwakilisha nchi yake kwa mara ya kwanza kwenye benchi la ufundi akiwa kama kocha kwenye dimba la Krasnodar.
Loading...

No comments: