Giroud atua Russia na bandeji - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, June 11, 2018

Giroud atua Russia na bandeji


Paris, Ufaransa. Mshambuliaji mahiri wa Ufaransa, Olivier Giroud licha ya kuzua hofu juu ya jeraha lake ameweza  kusafiri na wenzake hadi Russia tayari kwa fainali za Kombe la Dunia.
Giroud aliumia kichwani na kushonywa nyuzi sita, baada ya kugongana na mchezaji mwenzake wa klabu ya Chelsea, Matt Miazga, wakati Ufaransa ikicheza mechi ya mwisho ya kujipima nguvu dhidi ya Marekani, mchezo ulioisha kwa sare ya bao 1-1.
Kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, amesema walitishika sana alipoumia, lakini matabibu wawamesema mshambuliaji huyo atacheza mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia dhidi ya Australia.
“Ni kweli Olivier Giroud ameumia kichwani na kushonywa nyuzi sita, lakini yupo vizuri tunaamini atakuwepo katika mechi yetu ya kwanza dhidi ya Australia,” alisema Deschamps.
Ufaransa iliyo kundi C, inatarajiwa kuanza kutupa karata yake Jumamosi hii Juni 16, kwa kucheza dhidi ya Australia.
Baada ya kukipiga na Australia, Ufaransa mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka 1998 itacheza na Peru na Denmark, katika mechi za makundi za kinyang’anyiro hicho.


KWA HISANI YA MWANANSPOTI

Loading...

No comments: