Hispania yamtimua kocha wake, Julen Lopetegui siku moja kabla ya kombe la dunia - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, June 13, 2018

Hispania yamtimua kocha wake, Julen Lopetegui siku moja kabla ya kombe la dunia

Chama cha soka nchini Hispania kimemtimua kocha wake, Julen Lopetegui hii leo ikiwa imesalia siku moja pekee kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la Dunia nchini Urusi.

Lopetegui mwenye umri wa miaka 51 ameondolewa kwenye nafasi hiyo mara baada ya hapo jana kutangazwa na klabu ya Real Madrid kuchukua mikoba ya Zinedine Zidane aliyeachana na kibarua cha kuendelea kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria wa klabu bingwa barani Ulaya.
Rais wa chama hicho chenye dhamana ya kusimamia mchezo wa soka Hispania, Luis Rubiales ametangaza kuachana na kocha huyo na kumtakia kila lakheri kwenye majukumu yake mapya.
Rubiales amesema kuwa mazungumzo ya Lopetegui na Madrid yamefanyika pasipo kushirikisha chama hicho cha soka na kuelezwa dakika tano kabla ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari.
Timu ya taifa ya Hispania inatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa kundi B dhidi ya Ureno siku ya Ijumaa ya wiki hii majira ya asubuhi.

Loading...

No comments: