KAMATI YA BUNGE YA KUCHUNGUZA RASILIMALI ZA GESI ASILIA YABAINI UPOTEVU WA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 200 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, June 2, 2018

KAMATI YA BUNGE YA KUCHUNGUZA RASILIMALI ZA GESI ASILIA YABAINI UPOTEVU WA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 200
Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge ya Gesi Asilia, Dunstan Kitandula amesema wamebaini madudu yanayoisababisha Serikali hasara ya Sh291bilioni sawa na bajeti ya wizara nne, akiwemo mfanyakazi mmoja wa kampuni ya Payeti anayelipwa mshahara wa Sh 96 milioni kwa mwezi.

Hayo yamebainishwa na kamati hiyo iliyochunguza rasilimali za gesi asilia iliyoundwa na Spika Job Ndugai ambayo leo Jumamosi Juni 2, 2018 imewasilisha taarifa yake ya uchunguzi kwa kiongozi huyo wa Bunge mjini Dodoma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya taarifa za kamati hiyo, Kitandula amesema wamebaini kuwepo kwa baadhi ya wafanyakazi kutoka nje ya nchi wanaolipwa mishahara mikubwa kwenye kampuni hizo ikilinganishwa na Watanzania.
Akipokea Ripoti zote mbili Spika wa Bunge Job Ndugai amesema, Bunge limekamilisha kazi yake iliyobakia ni jukumu la serikali kuyafanyia kazi mapendekezo hayo huku kaimu kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni Prof Makame Mbarawa akisema kuwa serikali itayafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati hizo.

Kitandula ameongeza kuwa baadhi ya masharti kikwazo yaliyopo katika mikataba hiyo ni pamoja na tozo na ada mbalimbali, vifungu vinavyolazimisha akaunti za kampuni hizo kufunguliwa nje ya nchi na  utaratibu wa kutatuliwa migogoro nje ya nchi na sharti.
Na Amos C Nyanduku

Loading...

No comments: