Kilichowakuta Ujerumani hakijawahi kuwapata tangu 1938 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 28, 2018

Kilichowakuta Ujerumani hakijawahi kuwapata tangu 1938

Miaka 80 iliyopita(1938) ndio ilikuwa mara ya mwisho kwa Ujerumani kutolewa kombe la dunia wakati katika hatua ya makundi, na hii leo kipigo cha 2-0 kutoka kwa Korea kinawatoa tena kombe la dunia katika hatua ya makundi.
Hii ni kama laana ya kubeba ubingwa wa kombe la dunia, kwani katika misimu miwili mfululizo iliyopita bingwa wa kombe la dunia alitolewa katika makundi kwenye michuano iliyofuata(Italia 2010 na Hispania 2014).
Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Ujerumani kupigwa na timu kutoka Asia, katika mara zote 5 ambazo  Ujerumani walikutana na timu kutoka Asia katika kombe la dunia walishinda na wakiwa na ujumla ya ushindi wa mabao 19-3.
Mexico 0 – Sweden 3. Andreas Granqvist aliifungia Sweden mabao 2+ na sasa anakuwa Msweden wa pili kufunga mabao 2 kwa Sweden katika kombe la dunia tangu Henrik Larson afanye hivyo mwaka 2002.
Edson Alvarez alijifunga goli na hili linakuwa goli la 7 la kujifunga katika michuano hii ya kombe dunia, inakuwa michuano ambayo hadi sasa ina mabao mengi zaidi ya kujifunga.
Kwa matokeo haya sasa Sweden anafudhu kwenda 16 bora huku wakiwa vinara wa kundi F wakifuatiwa na Mexico, Korea wanamaliza nafasi ya tatu huku Ujerumani wakiburuza mkia.KWA HISANI YA SHAFFIH DAUDA
Loading...

No comments: