MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MMILIKI JAMII FORUMMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na Mwanahisa wa  mtandao huo, Micke William baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa aliwaachia huru washtakiwa hao leo Juni 1, baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka na kuona ushahidi huo hauna mashiko.

Hakimu Mwambapa amesema, hakukuwa na ushahidi unaoeleza moja kwa moja wa barua hiyo ya kuwataka watoe taarifa za kampuni yao na ushahidi huo una mashaka

Katika kesi hiyo Melo na mwenzake wanadaiwa kuzuia uchunguzi wa jeshi la polisi kwa kukataa kutoa taarifa za kampuni yao.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa,amedai kuwa baada ya usajili, kampuni hupewa taarifa za siri ambazo huwezesha mtu kuingia katika mtandao huo husika hivyo washtakiwa hao walikuwa na uwezo kuona taarifa kwenye mfumo wao.

Na Amos Nyanduku

Post a Comment

0 Comments