MamboSasa: Dr Shika Hana Hela Yoyote, Ni Muongo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, June 13, 2018

MamboSasa: Dr Shika Hana Hela Yoyote, Ni Muongo

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema kuwa Dk. Shika anacheza na akili za watu na hana fedha yoyote aliyopeleka benki kama alivyodai.

Akizungumza na Redio Times Fm, leo Juni 13, 2018 amesema kuwa kwa mara ya mwisho alisema fedha zimeingia benki lakini hana fedha.

Kauli hiyo imekuja baada ya kuulizwa kuwa kuna taarifa kuwa Dk. Shika amepata fedha zake, hizi taarifa zikoje mmempa ulinzi wa kutosha wakati wa kupokea?

“Dk. Shika anaendelea kucheza na akili za watu , hana fedha amepata lini yule mzee wa madau anapiga dau kubwa lakini kwa madhumuni yake binafsi, kwa mara ya mwisho alisema fedha zimeingia benki, benki gani hamna chochote , hana fedha,” amesema Kamanda Mambosasa.

Umaarufu wa Dkt. Shika umekuja baada ya kujitokeza katika mnada wa kuuza nyumba za Lugumi ambapo Dk. Shika aliahidi kununua nyumba hizo kwa thamani ya Sh. bilioni 2.3 lakini alishindwa kulipia asilimia 25 ya fedha hizo ambazo ni shilingi milioni 800.
Loading...

No comments: