MANISPAA YA KINONDONI YAINGIA MKATABA WA BILIONI 39 UJENZI WA MIUNDOMBINU KINONDONI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, June 2, 2018

MANISPAA YA KINONDONI YAINGIA MKATABA WA BILIONI 39 UJENZI WA MIUNDOMBINU KINONDONIManispaa ya Kinondoni imeingia makubaliano ya ujenzi wa barabara zenye thamani ya Milioni 39.062 zinazotarajia kujegwa katika Kata ya Tandale, Mburahati pamoja na Mwananyamala.

Akizungumza katika hafla ya kutiliana sahihi ya Mikataba ya Ujenzi baina ya serikali na wakandarasi, Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Kinondoni Aron Kagurumjuli amesema kuwa Kampuni ya CRJE East Africa Ltd na China Railway South Group Co. Ltd zimefanikiwa kushinda zabuni katika mradi huo.

Amesema kuwa mradi wa awamu  ya tano utatekelezwa na kampuni ya CRJE huku mradi wa sita utajegwa na China Railway Group Co.Ltd.

Kagurumjuli ameeleza kuwa ujenzi wa barabara hizo itakuwa katika kiwango cha Lami, mifereji, Taa, njia za watembea kwa mguu pamoja na vyoo katika Kata ya Tandale na Mburahati.

Amefafanua kuwa tayari wakazi wote wa maeneo hayo ambayo mradi huo utapita wamelipwa fidia, hivyo wakandarasi muda wowote kuanzia sasa wanaanza kazi.

Akizungumza katika hafla hiyo Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sitta, amesema kuwa serikali itaendelea kuwajali wananchi wake kwa kuhakikisha inaboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara.

Sitta amaeleza kuwa serikali inatumia gharama kubwa katika kujenga mradi wa barabara, hivyo wakandarasi wanapaswa kufanya kazi kwa kiwango kinachostahili.

Hata hivyo ameishukuru serikali Kuu pamoja na Ofisi ya Rais  kwa kufanikisha mradi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Happy, amesema kuwa fedha za kutekeleza mradi wa barabara serikali imekopwa na hivyo wandarasi wa ujenzi miundombinu hiyo wanapaswa kufanya kazi kwa weredi ili kuhakikisha fedha inatumika kama ilivyokusudiwa.

Na Amos C Nyanduku


Loading...

No comments: