Marekani, Canada na Mexico kuwa waandaaji wa michuano ya kombe la dunia 2026 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 14, 2018

Marekani, Canada na Mexico kuwa waandaaji wa michuano ya kombe la dunia 2026  Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani (FIFA) limezitangaza nchi za Marekani, Canada na Mexico kuwa waandaaji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2026.
  Nchi hizo za Amerika Kaskazini zimepata nafasi hiyo baada ya kupata jumla ya kura 134 kati ya 203 zilizopigwa kwenye Mkutano huo wa FIFA uliyofanyika Moscow nchini Urusi huku Morocco ikiambulia 65.
  Mashindano hayo yajayo ya kombe la dunia yatashuhudiwa zaidi ya timu 48 kutoka 32 zilizopo sasa katika michuano hiyo.
  Jumla ya michezo 80 itapigwa kwenye michuano hiyo, 60 ikitarajiwa kufanyika Marekani huku 20 iliyobaki ikigawana nchi za Canada na Mexico wakati fainali ikipigwa dimba la MetLife lililopo New Jersey sehemu ambayo zinatokea klabu za New York Giants na New York Jets.
  Loading...

  No comments: