MBUNGE WA CHALINZE, RIDHIWAN KIKWETE AMEPOKEA MSAADA WA FUTARI KWA AJILI YA WANANCHI WA JIMBO LAKE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, June 3, 2018

MBUNGE WA CHALINZE, RIDHIWAN KIKWETE AMEPOKEA MSAADA WA FUTARI KWA AJILI YA WANANCHI WA JIMBO LAKE

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete (kushoto)  akipokea msaada wa futari kutoka kwa Arif  Yusuf wa Taasisi ya Dural Irshad Islamic Centre ya Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete amepokea msaada wa futari kutoka kwa taasisi mbili za kidini, kwa ajili ya waislamu waliopo kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani jimboni humo.
Akipokea msaada wa futari hiyo iliyotolewa na taasisi za Dar Irushad Islamia Markaz na Miraj Islamic Centre za jijini Dar es Salaam kwa ajili ya wananchi wasiojiweza, Ridhiwan Kikwete amesema msaada huo utawafikia walengwa na kuzishukuru taasisi hizo kwa kuwakumbuka wananchi wanaoishi katika mazingira magumukatika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
Na Amos C Nyanduku
Loading...

No comments: