MSAFARA WA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA WAPATA AJALI MBAYA MEATU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, June 11, 2018

MSAFARA WA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA WAPATA AJALI MBAYA MEATUMsafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James umepata ajali wilayani Meatu, Simiyu na inadaiwa kwamba mtu mmoja amefariki dunia huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kwamba chanzo cha ajali hiyo, ni gari la polisi lililokuwa kwenye msafara huo kuchomoka tairi na kusababisha magari mengine yaliyokuwa kwenye msafara, kugongana huku basi la Rombo nalo likiligonga moja kati ya magari yaliyokuwa kwenye msafara.
Inaelezwa kwamba majeruhi wa ajali hiyo iliyotokea katika Kijiji cha Kisesa, wamekimbizwa katika Hospitali ya Mwandoya kwa matibabu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Boniventure Mshongi alipoulizwa kuhusu ajali hiyo, alisema bado hana taarifa kamili kwa kuwa yuko kwenye ziara ya kikazi. Juhudi za kumpata Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa.
Na Amos C Nyanduku
Loading...

No comments: