MTIBWA YATWAA UBINGWA WA KOMBE LA FA KWA KUIFUNGA SINGIDA 3-2 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, June 2, 2018

MTIBWA YATWAA UBINGWA WA KOMBE LA FA KWA KUIFUNGA SINGIDA 3-2

Mtibwa Sugar wametangazwa rasmi kuwa mabingwa wa Kombe la Shirikisho baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United katika mchezo wa fainali uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Bao la Kiwimbwa lilidumu kwa dakika 15 tu ambapo katika dakika ya 37 Mtibwa walijipatia bao la pili kupitia kwa Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ aliyefunga kwa mpira wa kona ulioenda moja kwa moja langoni na kumuacha kipa Ally Mustafa wa Singida United akiwa hana la kufanya.
Wakati dakika 45 za kwanza zikielekea kumalizika huku ubao wa matokeo ukisomea ni 2-1, Singida walipata nafasi ya kuandika bao la kwanza likitiwa kimiani na Chuku kwenye dakika ya 43, mpaka Mwamuzi anapuliza kipyenga kuashiria mapumziko, matokeo yalikuwa ni 2-1.
Kipindi cha pili kilianza tena kwa kasi huku Singida wakilishambulia zaidi lango la Mtibwa Sugar, na katika dakika ya 71 ya mchezo, mshambuliaji wa timu hiyo Tafadzwa Kutinyu aliisawazishia na kubadilisha ubao wa matokeo kwa kusomeka 2-2.

Na Amos C Nyanduku
Loading...

No comments: