Neymar, Brazil watua kibabe Russia - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, June 11, 2018

Neymar, Brazil watua kibabe RussiaBrazil ilitua alfajili ya leo jiji Sochi, na kufikia katika hoteli iliyofukweni mwa Black Sea wakipumzika hapo baada ya kumchapa Austria 3-0 katika mchezo wa mwisho wa maandalizi yao ya Kombe la Dunia.

Moscow, Russia. Kikosi cha Brazil kimewasili Russia leo asubuhi huku nyota wake Neymar akionekana amepona kabisa mguu wake jeraha lake na sasa yupo tayari kusaka ubingwa wa sita wa Kombe la Dunia.
Brazil ilitua alfajili ya leo jiji Sochi, na kufikia katika hoteli iliyofukweni mwa Black Sea wakipumzika hapo baada ya kumchapa Austria 3-0 katika mchezo wa mwisho wa maandalizi yao ya Kombe la Dunia.
Neymar alianza kwa mara ya kwanza katika mchezo huo baada ya kuwa nje kwa miezi mitatu, alifunga katika mchezo huo uliofanyika mjini Vienna huku mabao mengine yakifungwa na Gabriel Jesus na Philippe Coutinho.
Hilo ni bao 55 kwa Neymar akiwa na jezi ya Brazil na kumfanya kuifikia rekodi ya Romario na sasa amezidiwa na Pele na Ronaldo wachezaji waliofunga mabao mengi zaidi wakiwa na timu ya taifa.

Brazil itaanza kampeni yake dhidi ya Uswisi mjini Rostov-on-Don hapo Jumapil


HABARI KWA HISANI YA MWANASPOTI ONLINE
Loading...

No comments: