Nguruwe, Mystic Marcus aliyetabiri ushindi wa Trump azitabiria makubwa timu hizi kombe la dunia - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, June 15, 2018

Nguruwe, Mystic Marcus aliyetabiri ushindi wa Trump azitabiria makubwa timu hizi kombe la dunia

Wakati michuano ya kombe la dunia ikiwa imeanza nchini Urusi kumeibuka mnyama aina ya Nguruwe ambaye anatabiri mechi mbalimbali zinazoendelea kwa sasa na hivyo kuzua gumzo kubwa miongoni mwa wapenda soka.Inadaiwa kuwa Nguruwe huyo anayejulikana kwa jina la Mystic Marcus utabiri wake kwenye michezo ni wa asilimia 100 hii ni kwa mujibu wa mmiliki wa mnyama huyo Juliette Stevens .
Hata hivyo ni habari mbaya kwa timu ya taifa ya Uingereza baada ya Nguruwe huyo, Marcus kuzitabiria Ubelgiji, Argentina, Nigeria na Uruguay kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia kwa mwaka huu 2018.
Stevens amesema kuwa Marcus alipatia wakati alipotabiri mshindi wa michuano hiyo mwaka 2014, bingwa wa taji la mchezo wa tennis la Wimbledon, Brexit na ushindi wa Donald Trump kuwa rais wa taifa la Marekani.
Juliette ambaye anatokea Heage amesema kuwa Marcus ni mtoto wa saba kwenye watoto saba waliyozaliwa na wazazi wake na uwezo aliyokuwa nao ni kama zawadi.
Nguruwe huyo hutumia tunda aina ya appple katika kufanya utabiri wake na anajumla ya watoto na wajukuu 30 .

Loading...

No comments: