RAIS MAGUFULI AMETUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MAPACHA WALIOUNGANA, MARIA NA CONSOLATA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, June 3, 2018

RAIS MAGUFULI AMETUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MAPACHA WALIOUNGANA, MARIA NA CONSOLATAKufuatia kifo cha mapacha walioungana, Maria na Consolata Mwakikuti, waliofariki dunia usiku wa Juni 2, 2018 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kutokana na matatizo katika njia ya hewa yaliyokuwa yakiwasumbua, Rais Dkt John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa wote walioguswa na msiba huo.

Katika salamu zake za rambirambi kwa familia, watawa wa Kituo cha Maria na Consolata na wote walioguswa na msiba huo, Rais Magufuli amesema kabla ya kufikwa na mauti, walikuwa na ndoto ya kulitumikia taifa na kuwaombea wapumzike mahali pema peponi.

Naye mganga mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Museleta Nyakaloto amesema watoto hao waliopokelewa Mei 17, mwaka huu wakitokea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, walikuwa wakisumbuliwa na tatizo la upumuaji na wametibiwa hospitalini hapo kwa zaidi ya wiki mbili.

Na Amos C Nyanduku
Loading...

No comments: