Rais Magufuli ateua msajili wa vyama vya siasa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 21, 2018

Rais Magufuli ateua msajili wa vyama vya siasa


==
Mapema Leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemteua Bw. Mohammed Ali Ahmed kuwa Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Bw. Mohammed Ali Ahmed umeanza leo tarehe 20 Juni, 2018.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Mohammed Ali Ahmed alikuwa mwanasheria na mtafiti katika Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar.

Bw. Mohammed Ali Ahmed amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Rajab Baraka Juma ambaye amestaafu.==

Loading...

No comments: