RAIS MAGUFULI KUMPOKEA RAIS MNANGAGWA WA ZIMBABWE LEO. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 28, 2018

RAIS MAGUFULI KUMPOKEA RAIS MNANGAGWA WA ZIMBABWE LEO.


Nchi yetu imepata heshima ya kupokea ugeni wa Mhe. Emerson Mnangagwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Zimbabwe ambaye anatarajiwa kufika hapa nchini siku ya Alhamis tarehe 28/06/2018 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 28/06/2018 hadi 29/06/2018. Mhe. Mnagangwa atapokelewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport Terminal I na mwenyeji wake hapa nchini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli muda wa saa 5.00 asubuhi. Ikumbukwe kuwa hii itakuwa ni ziara ya kwanza kwa Rais Mnagangwa kufika Tanzania kama Rais tokea aingie madarakani mwishoni mwa mwezi Novemba, 2017. Ujio huu wa Rais Mnagangwa hapa nchini una lengo kuu la kuendelea kudumisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo baina ya nchi yetu na nchi ya Zimbabwe tangia wakati wa kupigania Uhuru wa Taifa hili la Kusini mwa Afrika. Mgeni wetu anatarajiwa kuondoka hapa nchini tarehe 29/06/2018 saa 8.00 mchana na atasindikizwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Kwa kutambua ugeni huu sisi kama wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa niaba ya wananchi wote wa Tanzania tunawakaribisha wageni wetu na wajisikie kuwa wako nyumbani muda wote watakapokuwa hapa jijini. Asanteni sana. Paul C. Makonda
Loading...

No comments: