SERIKALI YATOA ONYO KWA WANAOFANYA BIASHARA YA UTALII KINYUME CHA SHERIA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 21, 2018

SERIKALI YATOA ONYO KWA WANAOFANYA BIASHARA YA UTALII KINYUME CHA SHERIA

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Simu Na: +255 026 2321566
Nukushi: +255 026 2321514
Barua pepe: ps@mnrt.go.tz
      Description: tanzania-coat-of-arms-png
Mtaa wa Kilimani,
Barabara ya Askari,
S.L. P 1351,
40472-DODOMA
Description: TAARIFA-PRESS-ILLUSTRATOR

ONYO KWA WANAOFANYABIASHARA YA UTALII KINYUME CHA SHERIA

Hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la watu na makampuni yanayofanya biashara ya utalii kinyume cha sheria ikiwemo kutokuwa na Leseni ya Biashara za Utalii (TTBL). Watu hao pia wamekua wakijihusisha na vitendo vya utapeli na udanganyifu kwa watalii na hivyo kusababishia usumbufu mkubwa pamoja kuharibu taswira ya sekta ya utalii na Taifa kwa ujumla.

Tunaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuweza kuwabaini wote wanaohusika na vitendo hivyo ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria na iwe fundisho kwa wengine. Sheria ya Utalii Na. 29 ya mwaka 2008 Kifungu cha 10, 21 na 31(1-6) inamtaka mtu yeyote anayefanya biashara ya utalii kusajili na kulipa Ada ya Leseni ya Biashara ya Utalii kwa mwaka husika.

Tunasisitiza umma, watalii na wadau wa utalii kwa ujumla kufanya biashara na kampuni zilizosajiliwa na Mkurugenzi wa Utalii na kupewa leseni na Bodi ya Leseni ya Biashara za Utalii kuepuka kutapeliwa na usumbufu mwingine utakaoweza kujitokeza.

Aidha, wafanyabiashara wa utalii, wapya na wale wanaoendelea na biashara, wanajulishwa kuwa maombi ya usajili na utoaji wa leseni za biashara za utalii kwa mwaka 2018 yanaendelea kupokelewa. Ni kosa kisheria kuwasilisha taarifa za uongo na adhabu yake ni pamoja na kufutiwa leseni.

Orodha ya wakala wa biashara ya utalii waliosajiliwa na wenye leseni ya kufanya biashara ya utalii mwaka 2018 inapatikana kwenye tovuti yetu ya Wizara, www.mnrt.go.tz katika kipengele cha wadau (Stakeholders – Tour operators).

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu ya Wizara, www.mnrt.go.tz  au fika katika ofisi zetu za Makao Makuu zilizopo Mtaa wa Kilimani, Barabara ya Askari - Dodoma au Ofisi za Utalii za Kanda zilizopo Jengo la Mpingo - Dar es Salaam; New Mwanza Hotel - Mwanza; Jengo la NSSF - Iringa na TANAPA Makao Makuu - Arusha.
Maj. Gen. Gaudence Milanzi
KATIBU MKUU

21 Juni, 2018
Loading...

No comments: