Singida United wawaangamiza wababe wa Yanga, wajishindia mamilioni ya fedha kutoka SportPesa Super Super Cup (+video) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, June 11, 2018

Singida United wawaangamiza wababe wa Yanga, wajishindia mamilioni ya fedha kutoka SportPesa Super Super Cup (+video)

Klabu ya Singida United kutoka Tanzania imefanikiwa kuichabanga klabu ya Kakamega HomeBoyz goli 4-1 kwa njia ya mikwaju ya penati baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 za kawaida.
Kakamega ambao ndio walianza kupata goli kunako kipindi cha kwanza cha mchezo walifunga goli moja tu kwenye hatua hiyo ya mikwaju ya penati kati ya 4 walizopiga huku Singida wakipata penati zote 4 walizopiga.
Ikumbukwe kuwa Kakamega ndio walioitoa klabu ya Yanga kwenye mchezo wa kwanza wa michuano hiyo yenye msisimko zaidi Afrika Mashariki.
Kwa ushindi huo Singida United inachukua ushindi wa nafasi ya tatu ambapo itarudi nyumbani na kitita cha dola $7,500 sawa na tsh milioni 17.Tazama magoli yote ya penati hapa chini
Loading...

No comments: