Spika wa bunge Job Ndugai ameitaka serikali kufanyia kazi
ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na wabunge wakati wa mkutano wa 11 wa bunge
la bajeti ili kuwaletea maendeleo
wananchi.
Spika Ndugai Ametoa kauli
hiyo wakati akihairisha bunge hilo leo jijini Dodoma huku akisema kuwa bunge la
11 litakumbukwa kama bunge la korosho na kuongeza kuwa wizara ya kilimo
imehaidi kusimamia kikamilifu suala hilo.
Pia Spika Ndugai
amethibitisha kuwa tayari kiasi cha shilling million 7 laki 8 na 40 elfu kilichochangishwa na wabunge kwaajili ya
maharusi wa mfano kutoka jimbo la liwale bwana na bibi Jivunie Mbunda tayari
fedha hizo zimeshakabidhiwa kwa wahusika , hata hivyo bunge hilo limehairishwa
leo juni 29 hadi September 4, mwaka huu.
Na Amos
Nyanduku
0 Comments