Tamko la Brazil baada ya Neymar kutofanya mazoezi - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, June 20, 2018

Tamko la Brazil baada ya Neymar kutofanya mazoezi


Shirikisho la soka nchini Brazil CBF limeweka wazi kuwa nyota wa timu Neymar Jr hajafanya mazoezi ya Jumatatu na wenzake kutokana na kuwa na programu maalum na daktari wa timu hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya nyota huyo pamoja na wenzake wawili Paulinho na Thiago Silva, kukosa mazoezi ya Jumatatu na badala yake kukaa na watalaam wa afya kwaajili ya uchunguzi iwapo wamepata amajeraha.

CFB imesema kwa mujibu wa daktari wa timu Rodrigo Lasmar, Neymar na wenzake hawana shida yoyote na ni kawaida kwa wachezaji kuangaliwa hali yao na watalaam wa maabara ili kuepusha kuwaweka kwenye hatari iwapo wana maumivu.

Neymar alifanyiwa faulo mara 10, katika mchezo dhidi ya Switzerland uliopigwa Jumapili na kumalizika kwa sare ya 1-1. Ikumbukwe kuwa Neymar Jr aliumia mguu wa kulia kwenye klabu yake ya PSG mwezi Februari hali iliyopelekea kukosa raundi ya pili.

Brazil itarejea uwanjani tena leo  Jumatano kucheza na Serbia kwenye mechi yake ya pili katika kundi E. Mpaka sasa Serbia wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 3 baada ya kuanza kwa ushindi dhidi ya Costa Rica.

Loading...

No comments: