Tazama matukio katika picha kutoka Bungeni Jana – June 13, 2018 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 14, 2018

Tazama matukio katika picha kutoka Bungeni Jana – June 13, 2018


Kikao cha 50, mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea Jijini Dodoma, Leo Bunge limeongozwa na Mwenyekiti wa Bunge, Azzan Zungu. Kipindi cha Maswali na Majibu kiliendelea na wabunge walihoji maswali na kujibiwa na Serikali.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo wakati wa kuchangia hoja ya iliyowasiliwashwa na Mbunge Boniphace Simbachawene(hayupo pichani) kwa niaba ya wabunge wa Mkoa wa Dodoma wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Kibakwe wilayani Mpwapwa George Boniphace Simbachawene akiwasilisha hoja kwa niaba ya wabunge wa Mkoa wa Dodoma ya kuazimia Bunge litoe pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kuupa hadhi mji wa Dodoma kuwa Jiji wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akifafanua jambo wakati wa kuchangia hoja
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Mtamaa Nape Moses Nnauye wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa(kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wabunge wanawake na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) wakiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Mama Gaudensia Kabaka (mwenye mvi kichwani) walipotembelea Bungeni wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma
Loading...

No comments: