TETESI ZA USAJILI: Pochettino kumrithi Zidane - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, June 1, 2018

TETESI ZA USAJILI: Pochettino kumrithi ZidaneIkiwa ni muda mchache umepita tangu aliyekuwa kocha wa mabingwa wa Ulaya Real Madrid Mfaransa Zinedine Zidane atangaze kujiuzulu kuwanoa miamba hao.

Mauricio Pochettino wa Tottenham amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kubeba mikoba ya Zidane, mbali na Pocchetino orodha ya wengine wanaptajwa ni pamoja na  Massimiliano Allegri na Joachim Low.
Uamuzi wa Zidane ulileta  mawimbi na  mshtuko kote ulimwenguni baada ya kutangaza ghafla kuwa  anaondoka  klabuni hapo  ambapo ameshinda mataji matatu ya klabu bingwa barani Ulaya.

Zidane anakuwa kocha wa kwanza chini ya uongozi wa Rais wa klabu hiyo Perez kuondoka bila ya kufukuzwa Santiago Bernabeu. .


Loading...

No comments: