TFF YARIDHISHWA MAANDALIZI YA FAINALI ASFC,YASHUKURU WADAU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, June 4, 2018

TFF YARIDHISHWA MAANDALIZI YA FAINALI ASFC,YASHUKURU WADAU






Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) limeridhishwa na maandalizi yaliyofanikisha mchezo wa Fainali ya Azam Sports Federation Cup ikiwa pamoja na kuwashukuru Wadau mbalimbali.

Fainali hiyo iliyowakutanisha Mtibwa Sugar na Singida United ilikuwa ya aina yake kwa ushirikiano wa TFF na Wadau mbalimbali.

TFF inachukua nafasi hii kuishikuru Serikali ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Mrisho Gambo kwa kuwa sehemu ya kufanikisha Fainali hiyo.

Pia TFF inamshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndugu Athuman Kihamia,Wananchi wa Arusha na mashabiki waliosafiri kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo mikoa ya jirani kushuhudia mchezo huo wa Fainali.

Vilevile TFF inatoa shukrani za dhati kwa Azam Tv Wadhamini wakuu wa Azam Sports Federation Cup kwa msimu wa tatu sasa na pia tunatoa shukrani kwa wadhamini waliojitokeza kwenye mchezo wa Fainali Benki ya KCB.

Kwenye mchezo huo wa Fainali Mtibwa Sugar walifanikiwa kutwaa Ubingwa baada ya kuifunga Singida United kwa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,Arusha.

Mtibwa Sugar wamezawadiwa medali,fedha shilingi milioni 50 na Kombe wakati Singida United kwa kumaliza nafasi ya pili wamepata medali na fedha shilingi milioni 10.
Loading...

No comments: