Ufaransa Yatinga 16 Bora Kombe la Dunia....Ni Baada ya Kuitandika Peru 1-0 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, June 22, 2018

Ufaransa Yatinga 16 Bora Kombe la Dunia....Ni Baada ya Kuitandika Peru 1-0

Bao pekee la Kylian Mbappe limewafanya Ufaransa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Peru katika mchezo wa kundi C kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi.

Mbappe amefunga bao hilo akiwa na umri mdogo zaidi kwenye michuano hiyo mnamo dakika ya 34 ya kipindi cha kwanza na kudumu dakika zote za mchezo.

Mchezaji huyo anayeichezea PSG ya Ufaransa amefunga bao hilo la kwanza ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki mashindano hayo akiwa na umri wa miaka 19 na miezi 6 pekee.

  
Kwa matokeo hayo, timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa  moja kwa moja kuingia hatua ya 16 bora na kuiondosha Peru kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka huu.

Ufaransa iliyopo kundi C inafikisha pointi 6 ikifatiwa na Denmark yenye pointi 4 ambayo inahitaji pointi moja ili kuungana na Ufaransa au ikiomba Peru anayeburuza mkia wa kundi hilo kwa kutovuna pointi hata moja kwenye mchezo yake miwili amfunge Australia mwenye pointi moja kwenye mchezo wa kukamilisha ratiba ya kundi hilo.
Loading...

No comments: