Uruguay Yaichapa Saudi Arabia bao 1-0 Na Kutinga 16 Bora Kombe La Dunia - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 21, 2018

Uruguay Yaichapa Saudi Arabia bao 1-0 Na Kutinga 16 Bora Kombe La Dunia


Bao pekee katika mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay dhidi ya Saudi Arabia, limehitimisha safari ya michuano hiyo kwa Misri inayoongozwa na Mohamed Salah.
  
Uruguay imeshinda kwa bao 1-0 dhidi ya Saudi Arabia, shujaa akiwa ni Luis Suarez aliyewahi kuichezea Liverpool akiwa shujaa wa klabu hiyo, wakati huo.

Salah na Misri watapanda ndege kurejea nyumbani baada ya mechi yao ya mwisho ya kundi ikiwa ni ya kukamilisha.

Ushindi wa jana umeipa Uruguay pointi sita na kujihakikishia kusonga hatua ya mtoano pamoja na wenyeji Urusi huku Misri na Saudi Arabia, wakitupwa nyumbani.

Loading...

No comments: