Urusi yaingia kwenye rekodi nyinginekomb - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 14, 2018

Urusi yaingia kwenye rekodi nyinginekomb
Mchezaji wa timu ya Urusi Yury Gazinsky aibuka kuwa mfungaji wa bao la kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia kwa mwaka 2018 ambapo bao lake amelipashika mnamo dakika ya 12 za kipindi cha kwanza

Yury Gazinsky ameungana na wachezaji Neymar Jr wa Brazil na Siphiwe Tshabalala wa Afrika Kusini ambao wote walifunga mabao ya ufunguzi kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 na 2014.
Pia mchezaji Denis Cheryshev wa Urusi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutokea benchi na kufunga mabao mawili kwenye mechi hiyo ya ufunguzi huku mabao mengine yakiwa yamepachikwa na Aleksandr Golovin pamoja na Artem Dzyuba.
Kwa upande mwingine, wenyeji Urusi wamendeleza rekodi ya timu mwenyeji kutofungwa kwenye mechi ya ufunguzi tangu fainali hizo zianzishwe mwaka 1930 nchini Uruguay.
Loading...

No comments: