Urusi Yakabiliwa na Upungufu wa Bia, Mashabiki Walalamika - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, June 22, 2018

Urusi Yakabiliwa na Upungufu wa Bia, Mashabiki Walalamika


Urusi Yakabiliwa na Upungufu wa Bia, Mashabiki Walalamika
Nchini Urusi ambapo inadaiwa kuwa jiji la Moscow linakabiliwa na upungufu wa bia unaodaiwa kusababishwa na tabia ya baadhi ya Mashabiki waliyoenda kutazama Kombe la Dunia nchini humo kupenda kufakamia bia kwa wingi.

Kwa mujibu wa mashabiki waliopo katika jiji la Moscow wamenakiriwa wakilalamika kuwa wamekuwa wakisubiria kwa muda mrefu katika migahawa wanapoagiza bia kutokana na uhitaji wake kuwa mkubwa huku zikiwa chache.

Aidha nchi ya Urusi inatajwa kukamata nafasi ya 14 kwa unywaji wa bia duniani huku ikidaiwa kuwa uwepo wa mashabiki katika nchi hiyo walioenda kutazama kombe la Dunia umesaidia kunyanyua sekta ya bia nchini humo iliyokuwa inashuka.

Aidha mashabiki walioenda kushuhudia michuano hiyo wamevitaka viwanda vinavyotengeneza bia nchini humo kuongeza uzalishaji wa bia ili wasipate shida kuzipata 
Loading...

No comments: