VODACOM NA KWESE iflix WAZINDUA HUDUMA YA KUANGALIA MECHI ZA KOMBE LA DUNIA KIGANJANI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, June 13, 2018

VODACOM NA KWESE iflix WAZINDUA HUDUMA YA KUANGALIA MECHI ZA KOMBE LA DUNIA KIGANJANIMkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Plc, Nandi Mwiyombella akiongea  na waandishi wa habari (hawapo pichani)  jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi   wa Kampeni ya  cheki Kombe la Dunia  na Vodacom kwa kushirikiana na Kwese iflix  inayowawezesha  wateja wa mtandao wa Vodacom  kushuhudia michuano ya kombe la Dunia inayofanyika nchini Russia kwa  kupitia simu  za Kiganjani za smart phone kwa kupiga namba *149*01#  mteja atachagua Kwese iflix ili kupata vifurushi vya bando. Kushoto ni  Mkuu wa Kitengo cha Dijitali na huduma za ziada  wa Vodacom Tanzania, Paulina Shao na Mkurugenzi  wa Kwese TV, Mgope Kiwanga.

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Plc, Nandi Mwiyombella  (katikati) na   Mkuu wa Kitengo cha Dijitali na huduma za ziada wa  kampuni hiyo, Paulina Shao (kushoto) wakimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi  wa Kwese TV, Mgope Kiwanga  akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi   wa Kampeni ya  cheki Kombe la Dunia  na Vodacom kwa kushirikiana na Kwese iflix  inayowawezesha  wateja wa mtandao wa huo kushuhudia michuano ya kombe la Dunia inayofanyika nchini Russia kwa  kupitia simu zao za Kiganjani za smart phone kwa kupiga namba *149*01# Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Plc, Nandi Mwiyombella,  (wa tatu kushoto) na   Mkurugenzi  wa Kwese TV, Mgope Kiwanga   wakipongezana mara baada ya uzinduzi wa  Kampeni ya  cheki Kombe la Dunia  na Vodacom kwa kushirikiana na Kwese iflix  inayowawezesha  wateja wa mtandao huo  kushuhudia michuano ya kombe la Dunia inayofanyika nchini Russia  kupitia simu zao za Kiganjani za smart phone kwa kupiga namba *149*01#  mteja  anatachagua Kwese iflix kupata vifurushi vya bando. Kushoto ni Meneja Mkuu wa TV1, Joseph Sayi   na Mkuu wa Kitengo cha Digital na huduma za ziada Paulina Shao nameneja masoko wa Kwese iflix  Afrika Mashariki ,Bernice Macharia.


DAR ES SALAAM – Juni 13, 2018 – Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kwa mawasiliano kidijitali ya Vodacom kwa kushirikiana na Kwesé iflix, ambayo imeungana na Econet Media, kampuni ya utangazaji inayoongoza katika maeneo mengi ya bara la Afrika , leo wametangaza kuzinduliwa kwa mfumo wa kidijitali wa burudani utakaowezesha wateja wa Vodacom kuangalia mechi za kombe la Dunia moja kwa moja katika simu zao za mkononi.
Kwa kupitia mtandao wenye kasi kubwa ya 4G wa Vodacom, watumiaji wataweza kupata maudhui yenye ubora wa kimataifa kwa kasi kubwa kabisa bila kukwama wala kusita, hii itawawezesha kushuhudia mechi za kombe la Dunia zinazoanza kesho jijini Moscow nchini Urusi.
Huduma hii mpya kabisa ya Kwese iflix inawapa watumiaji burudani isiyo na mfano, ikijumuisha maudhui mapana ya Kwese ambayo ni pamoja na utangazaji mubashara wa mashindano makubwa kabisa ya kimataifa, pamoja na mashindano yajayo ya Kombe la Dunia 2018 kutoka Urusi- na mengine mengi zaidi kwenye jukwaa la kimataifa la Kwese ambapo kuna vipindi na programu bora kabisa za kimataifa, kikanda na kitaifa ambazo zimepangiliwa maalum kwa ajili ya watazamaji wa kiAfrika.

Ikiwa na maelfu ya vipindi, maktaba kubwa ya Kwese iflix ina mengi, pamoja na vipindi vya kimataifa vinavyoonyeshwa kwa mara ya kwanza, vipindi vya televisheni vilivyoshinda tuzo mbali mbali na sinema maarufu kama vile ICE, Cleverman, Project Runway; Fashion Start Up S1, Confess pamoja na vipindi vinavyopendwa vya ndani kama vile Muoshwa huoshwa, Barua, Mama Huruma, Nabii Mswahili & Saa Mbovu na maudhui ya kikanda - Telenovela kama vile Goblin, Naagin and Bride of Habaek – vipindi vya watoto na maudhui mengine ya kimaisha. Huduma hii pia inawapatia waTanzania maudhui bora watakayoweza kuangalia bila gharama, ikiwa ni pamoja na tamthilia na vipindi vingine vya televisheni.
Wakitangaza kuzinduliwa kwa huduma hii, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kwese iflix, Mayur Patel, alisema, “Ikiwa ni ushirikiano baina ya watengeneza vipindi na watangazaji, Kwese na iflix, app ya Kwese iflix inawapa wateja burudani bora kabisa wakati wowote na mahali popote. Huduma hii imebuniwa kwa kizazi cha kidijitali, watumiaji sasa wanaweza kufikia vipindi vyao waviupendavyo vya michezo na televisheni bila kikomo na kwa njia inayoendana na maisha yao – wakiwa katika mizunguko yao na kwa matakwa yao. Tunafurahishwa sana kushirikiana na Vodacom kufikisha maudhui yetu kwa waTanzania wengi zaidi.”

Kusherehekea uzinduzi huu, Vodacom inatoa ofa za kusisimua za data kwa bei nafuu. Vifurushi vya Kwese iflix vitawapatia wateja wa maudhui ya kulipiwa vya Kwese iflix na wateja wa Vodacom uwezo kujipatia huduma za video mtandaoni kwa masaa, kwa siku, kwa wiki na kwa mwezi. Kujipatia kifurushi cha data, wateja wa Vodacom watahitaji kupiga namba *149*01# > Internet > Video > Kwese ilfix. Wateja wanaweza kupakua app ya Kwese ilfix kwa urahisi kabisa kupitia Google Play au App Store.
Akizungumzia ushirikiano huu, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom  Bi Nandi Mwiyombella alisema, “Huduma za video ndiyo zitaongoza siku zijazo katika mawasiliano na Kwese iflix itatuwezesha kutoa maudhui bora kabisa za kimataifa na kitaifa za michezo na burudani kwa wateja wetu.”

Mmoja wa waanzilishi wa iflix na Afisa Mtendaji Mkuu, Mark Britt aliongeza, “Tukio hili ni kubwa sana kwa iflix. Kwa pamoja na Econet Media, kampuni ya utangazaji inayoongoza barani Afrika, tumebuni huduma mahususi kwa ajili ya watumiaji wa kiAfrika, huduma ambayo itawawezesha watumiaji nchi nzima kujionea kila mechi ya Kombe la Dunia kupitia vifaa vyao. Huduma yetu ya Kwese iflix sasa ina maktaba kubwa kabisa ya maudhui ya burudani bora duniani, vyote vikipatikana kwa wakati mtumiaji anapotaka, tofauti na zamani.”
“Hatuwezi kupuuzia ongezeko la huduma za video mtandaoni barani Afrika haswa tukizingatia ongezeko kubwa la watumiaji wa mawasiliano ya simu na mtandao. Tunalazimika siyo tu kuendana na muenendo bali kuhakikisha kuwa tunakuja kuwa watoa huduma bora kabisa sokoni. Kwese iflix inawapatia vijana mchanganyiko wa maudhui ya michezo na burudani na tunafurahia sana kuwa mstari wa mbele kwenye hili,” alisema Joseph Hundah, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Econet Media.
.
Watumiaji wa Kwese iflix wanaweza kuchagua kati ya pasi kadhaa za VIP ili kuweza kujipatia maudhui ya Kwese iflix ya kulipiwa, ikiwa ni pamoja nay a masaa mawili, siku moja, siku tatu, siku saba na siku 30.

Kwa maelezo zaidi juu ya ushirikiano wa Vodacom na  Kwese iflix
Loading...

No comments: