WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AMEWATAKA VIONGOZI WA DINI KUTOKUBALI KUCHONGANISHWA NA SERIKALI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, June 11, 2018

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AMEWATAKA VIONGOZI WA DINI KUTOKUBALI KUCHONGANISHWA NA SERIKALI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka viongozi wa dini kutowatumia watu tofauti nje ya taasisi zao kwa ajili ya kuwasemea kwani wanaweza kuwachonganisha na serikali yao.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa dini na wananchi wa Mkoa wa Mwanza baada ya kushirikiana nao katika futari aliyowaandalia, shughuli ambayo  ilihudhuriwa na waumini wa dini mbalimbali.
Majaliwa amesema kuwa serikali haiongozwi kwa misingi ya kidini bali imeziachia taasisi za kidini zifanye kazi kwa kuzingatia katiba, sheria za nchi na malengo yaliyokusudiwa katika uanzishwaji wake.
Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanaishi kwa amani na utulivu, jambo litakalowawezesha kufanya shughuli zao kikamilifu, hivyo wasikubali kuchonganishwa kwa misingi yoyote.
Na Amos C Nyanduku
Loading...

No comments: