Waziri Mpango: Akiba ya Fedha za Kigeni Imeongezeka na Kupita Viwango vya EAC - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 14, 2018

Waziri Mpango: Akiba ya Fedha za Kigeni Imeongezeka na Kupita Viwango vya EAC


Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango amesema akiba ya fedha za kigeni imeongezeka kwa mwaka 2017, na kupita viwango vilivyowekwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Amesema hayo leo bungeni alipokuwa akiwasilisha mwenendo wa uchumi kwa mwaka 2017.

Dk Mpango amesema akiba hiyo imeongezeka kutoka Dola 5.9 bilioni za Marekani zinazotosha kuagiza hiduma na bidhaa kwa miezi 5.1 kutoka Dola 4.3 bilioni za mwaka 2016.

Waziri huyo amesema EAC inazitaka nchi wanachama kuwa na akiba inayotosha miezi 4.5.
Loading...

No comments: