WCF YAWATAKA WAAJIRI KUFANYA TATHMINI YA VIWANGO HATARISHI SEHEMU YA KAZI MARA KWA MARA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 21, 2018

WCF YAWATAKA WAAJIRI KUFANYA TATHMINI YA VIWANGO HATARISHI SEHEMU YA KAZI MARA KWA MARA


Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakzi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, (kushoto), akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa waajri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri kufanya tathmini mara kwa mara ya viwango hatarishi mahala pa kazi.

Na mwandishi wetu, Tanga Juni 21, 2018
WAAJIRI wanao wajibu wa kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wao unapewa umuhimu wa kwanza na moja ya njia ya kutekelza hilo ni kufanya tathmni ya viwango hatarishi mara kwa mara.
Hayo yamesemwa leo Juni 21, 2018 na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Thathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa waajiri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri katika kuhakikisha usalama na afya ya mfanyakazi unazingatiwa.
Lakini pia aliwataka wafanyakazi nao watekeleza wajibu wao kwa kutumia vifaa kinga walivyopewa na waajiri wao pale wanapotekeleza majukumu yao ya kikazi ili kupunguza ajali zinazoweza kuzuilika.
Alisema ili kutekeleza awajibu huo wa kisheria, wajiri wanapaswa kufanya tathmini ya mara kwa mara ili kubaini vihatarishi mahala pa kazi ili kuchukua hatua ya kuzuia majanga yatokanayo na kazi.
“Ifahamike kuwa sisi WCF wajibu wetu wa msingi ni kulipa fidia stahiki na kwa wakati kwa mfanyakzi aliyeumia, kuugua au kufariki wakati akitekeleza wajibu wake wa kazi, ikiwa ni pamoja na kusajili na kupokea michango kutoka kwa waajiri walio katika sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara, lakini pia tunalo jukumu la kisheria la kukuza mbinu za kuzuia ajali na vifo kazini kwa kutoa elimu kwa waajiri lakini pia wafanyakazi wenyewe na hiki ndicho tunachokifanya hapa leo.” Alisema Dkt. Omary amabaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba.
Katika kuhakikisha wadau wanapata uelewa wa kutosha kuhusu majukumu ya Mfuko na wajibu wao katika kutekeleza sheria iliyoanzisha Mfuko, tumekuwa tukikutana na waajiri na kuwapa elimu kupitia semina kama hii ya leo, lakini pia tumekuwa tukitembelea maeneo ya kazi na kwa kushirikiana na waajiri wenyewe tumekuwa tukitoa elimu kwa wafanyakazi pia, alisema Mkurugenzi huyo wa hudumaz a Tiba na Tathmini.
“Na kwa hakika kumekuwepo na kukua kwa uelewa miongoni mwa waajiri, kuhusu shughuli za Mfuko, awali waajiri walidhani Mfuko kazi yake ni kusajili na kukusanya michango tu, lakini kupitia elimu hii tunayotoa kuhusu shughuli za Mfuko, kumekuwepo na mabadiliko makubwa, tumekuwa tukipokea maombi mengi kutoka kwa waajiri wakitaka tutembelee maeneo yao ya kazi, ili kutoa elimu hii kwa wafanyakazi pia, jambo ambalo hapo awaali wakati tunaanza halikuwepo na hakika kwetu sisi haya ni mafanikio.”
Dkt. Omary alisema, kwa sasa Mfuko umekuwa ukitekeleza majukumu yake kwa mafanikio makubwa ambapo zaidi ya waajiri 14,224 wamesajiliwa na wengine wapya wanaendelea kujisajili.
Mafaniukio mengine yaliyopatikana katika kipoindi kifupi, Mfuko umeweza kutekeleza jukumu lake la msingi la kulipa fidia satahiki na kwa wakati kwa wafanyakazi walioumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi kwa mafanikio makubwa.
“Pamoja na uchanga wake, Mfuko umeshalipa fidia  kiasi cha shilingi bilioni 2.52 kwa wafanyakazi walioumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi, haya ni mafanikio makubwa ambayo Mfuko umeyapata katika kipindi kifupi”.
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoanzishwa kwa mujibu kifungu namba 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura ya 263 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015, lengo kuu likiwa ni kulipa fidia stahiki na kwa wakati lakini pia kusajili na kukusanya michango kutoka kwa waajiri walio katika sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara.
Mfuko ulianzishwa mnamo mwaka 2015 na Serikali ilitoa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja ili kujiweka sawa na ilipofika Julai 2016 tulianza  kupokea madai ya fidia.
 Washiriki wakiendelea kuchukua nafasi zao.
 Baadhi ya washiriki wakisoma majarida ya WCF yenye maelezo mbalimbali kuhusu shughuli za Mfuko.


 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa WCF, Bi. Laura Kunenge, (katikati), Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi (kushoto) na Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. George Faustine wakipitia taarifa mwanzoni mwa mafunzo hayo.
 Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa WCF, Bi. Laura Kunenge, akiongoza mafunzo hayo.

 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakzi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, (kulia aliyesimama), akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa waajri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri kufanya tathmini mara kwa mara ya viwango hatarishi mahala pa kazi.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakzi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, (kushoto aliyesimama), akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa waajri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri kufanya tathmini mara kwa mara ya viwango hatarishi mahala pa kazi.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakzi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, (kulia aliyesimama), akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa waajri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri kufanya tathmini mara kwa mara ya viwango hatarishi mahala pa kazi. wengine pichani meza meza kuu ni, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi (kushoto) na Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. George Faustine
 Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. George Faustine, akizungumza.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
 Picha ya kwzna ya pamoja.
Picha ya pamoja ya pili.
Mshiriki (kulia), akipatiwa vipeperushi na vifaa vingine wezeshi vya mafunzo.
Mshiriki akijiandikisha.
Loading...

No comments: