Wimbo mwingine wa Rihanna wafikisha views Bilioni 1 YouTube - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, June 16, 2018

Wimbo mwingine wa Rihanna wafikisha views Bilioni 1 YouTube

RIHANA,YOUTUBE
Msanii wa muziki kutoka nchini Marekani, Rihanna amezidi kutamba vilivyo na ngoma zake katika mtandao wa YouTube.
Kupitia ngoma yake inayokwenda kwa jila la Work ambayo amemshirikisha Drake ameweza kufikisha views Bilioni 1 katika mtandao huo.

Video hiyo ambayo ilitoka February 22, 2016 si ya kwanza kutoka kwa Rihanana kufanya hivyo, kwani ngoma yake ‘Diamond’ ina views Bilioni 1.1 ambayo ilitoka November 08, 2012.
Utakumbuka March 09 mwaka huu katika kuhadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake duniani Apple Music ilitoa orodha ya wasanii 20 wa kike waliofanya vizuri katika stream ambapo Rihanna alifikisha wasikilizaji Billion mbili (2 billion steams) na kuwa msanii wa kwanza wa kike duniani kufanya hivyo.
Kwa sasa wimbo uliotamwa zaidi katika mtandao wa YouTube ni Despacito ya msanii kutoka katika visiwa vya Puerto Rico nchini Marekani, Luis Fonsi. Wimbo huo una views Bilioni tano na ulitoka Januari 12, 2017.
Loading...

No comments: