WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO KWA KUSHIRIKIANA NA TACAIDS INATANGAZA UZINDUZI WA KAMPENI YA FURAHA YANGU KUHAMASISHA HUDUMA ZA KUPIMA VVU NA KUANZA ARV MAPEMA. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, June 12, 2018

WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO KWA KUSHIRIKIANA NA TACAIDS INATANGAZA UZINDUZI WA KAMPENI YA FURAHA YANGU KUHAMASISHA HUDUMA ZA KUPIMA VVU NA KUANZA ARV MAPEMA.

D:\fhi Press\Dr. Angela Ramadhani.JPG
Kaimu Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Angela Ramadhani akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza mkakati wa uzinduzi wa  kitaifa wa kampeni ya FURAHA YANGU unao hamasisha watu tupima na kutibu ugonjwa wa ukimwi ijulikanayo kama Test and Treat campaign mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam leo. Mpango huu utazinduliwa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Jijini Dodoma tarehe 19 mwezi huu.
D:\fhi Press\Dr. Leonald Maboko.JPG
Mkuruugenzi Mtendaji wa tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza mkakati wa uzinduzi wa  kitaifa wa kampeni ya FURAHA YANGU unao hamasisha watu tupima na kutibu ugonjwa wa ukimwi ijulikanayo kama Test and Treat campaign mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam leo. Mpango huu utazinduliwa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Jijini Dodoma tarehe 19 mwezi huu. 

D:\fhi Press\Dr.Gissege Lija.JPG
Kaimu Meneja Mpango, NACP, Dkt. Gissege Lija, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza mkakati wa uzinduzi wa  kitaifa wa kampeni ya FURAHA YANGU unao hamasisha watu tupima na kutibu ugonjwa wa ukimwi ijulikanayo kama Test and Treat campaign mkutano uliofanyika  jijini Dar es salaam leo. Mpango huu utazinduliwa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Jijini Dodoma tarehe 19 mwezi huu.

D:\fhi Press\ILO - Jealous Chirove.JPG
Mtaalam wa maswala ya ajira-ILO, Jealous Chirove akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza mkakati wa uzinduzi wa  kitaifa wa kampeni ya FURAHA YANGU unao hamasisha watu tupima na kutibu ugonjwa wa ukimwi ijulikanayo kama Test and Treat campaign mkutano uliofanyika  jijini Dar es salaD:\fhi Press\Ananthy Thambinayagam.JPG

Kaimu Mkurugenzi wa maswala ya afya Afya wa USAID, Ananthy Thambinayagam akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza mkakati wa uzinduzi wa  kitaifa wa kampeni ya FURAHA YANGU unao hamasisha watu tupima na kutibu ugonjwa wa ukimwi ijulikanayo kama Test and Treat campaign mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam leo. Mpango huu utazinduliwa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Jijini Dodoma tarehe 19 mwezi huu.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP) kwa kushirikiana na TACAIDS  na wadau wa USAID Tulonge Afya, inayofuraha kutangaza uzinduzi wa kampeni ya kitaifa inayoitwa Furaha Yangu. Kampeni hii inahamasisha mkakati mpya wa serikali wa Upimaji wa VVU na kuanza kutumia ARV mapema kwa wale watakao kutwa na VVU. Kupitia Furaha Yangu, ujumbe  wa serikali ni kuwa kutambua hali yako ya VVU huleta amani, na kuanzishiwa ARV mapema kwa wale wenye VVU inawasaidia kuimarisha afya na  kupunguza hatari ya kuambukiza VVU kwa wenza wao.
Katika dira ya kuwa na Taifa bila UKIMWI, Tanzania imeridhia malengo ya UNAIDS ya 90-90-90: ambapo 90% ya watu wote wanaoishi na VVU kutambua hali zao za VVU, 90% ya watu wote wenye VVU kuanza ARV, na asilimia 90 ya wote walionza ARV kupunguza kiwango cha VVU mwilini. Uzinduzi wa kampeni ya furaha Yangu – ambayo imekuwa ikiandaliwa kwa mienzi kadhaa na Wizara kupitia NACP kwa kushirikiana na TACAIDS, mradi wa USAID Tulonge Afya na wadau wengine  ni mchango muhimu katika kutimiza malengo haya.
Kampeni ya furaha Yangu itazinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Mjaliwa Kassim Majaliwa (Mb), siku ya  tarehe 19 Juni 2018, katika Jiji la Dodoma ambayo pia ni kutakuwa na siku tano za kutoa huduma za afya bila malipo ikiwemo huduma ya upimaji wa VVU kuanzia tarehe 19 June 2018. Wizara kupitia NACP pamoja na TACAIDS inatoa wito kwa wakazi wote wa Jiji la Dodoma na mikoa ya jirani kushiriki katika uzinduzi huu na kupima afya zao na kuonyesha dhamira yao ya kumaliza VVU na UKIMWI nchini.


Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Simu: +255 – 026 - 2323267,S.L.B 743, Dodoma
Loading...

No comments: