Yanga yaondoka nchini kuelekea Kenya kwenye SportPesa Super Cup, Ajibu hajaonekana kocha afunguka (+video) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, June 1, 2018

Yanga yaondoka nchini kuelekea Kenya kwenye SportPesa Super Cup, Ajibu hajaonekana kocha afunguka (+video)


Wachezaji wa Yanga wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere jijini Dar es salaam tayari kuelekea Kenya.
Kikosi hicho ambacho baadhi ya nyota wake hawajaonekana uwanjani hapo akiwemo Ibrahim Ajib kimeondoka kikiwa na matumaini ya kufanya vizuri zaidi ingawaje kocha wa klabu hiyo, Zahera Mwinyi amedai kuwa michuano hiyo ni kama maandalizi kwao ya msimu mpya unao kuja.
Hata hivyo, viongozi wote wa Yanga wamekataa kuzungumzia kukosekana kwa Ajib kwenye kikosi hicho kilichoondoka jioni ya leo kuelekea Kenya.


CHANZO;Bongo5.com

Loading...

No comments: