Kampuni ya Uber imezindua namba za simu za dharura ambazo wasafiri wanaweza kutumia nchini Tanzania - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, July 19, 2018

Kampuni ya Uber imezindua namba za simu za dharura ambazo wasafiri wanaweza kutumia nchini TanzaniaTarehe 19 Julai 2018, Dar es Salaam…. Kampuni ya Uber nchini Tanzania ina furaha kuwantangazia rasmi hatua ilizochukua katika kuimarisha usalama; Namba za simu za Timu ya Matukio ya Dharura (IRT). Hii ni huduma mpya ambayo itawapa wasafiri wote nchini fursa ya kupata msaada kuhusu matukio ya kiusalama usiku na mchana kupitia Timu ya Matukio ya Dharura (IRT).
Kampuni ya Uber imeweka kipaumbele kwenye usalama wa madereva na wasafiri na ndio maana Uber ina mpango endelevu wa kuwekeza katika mikakati ambayo itaboresha huduma za app yake. Tayari wasafiri wanaweza kutumia mtandao mkubwa wa vituo vya huduma kwa wateja kupata msaada wanapohitaji usaidizi wowote usiku na mchana ndani ya programu. Kupitia namba hizi za Timu ya Matukio ya Dharura wasafiri wanaweza kupiga taarifa ya tukio lolote linalohatarisha usalama wao au ajali ndani ya app, kuandika namba zao za simu pamoja na maelezo machache kuhusu tukio hilo. Baadaye wasafiri watapigiwa simu na Timu ya Matukio ya Dharura (IRT) haraka iwezekanavyo.
Alfred Msemo, Meneja Msimamizi wa Uber nchini Tanzania, “Tunafanya kila juhudi ili kuboresha mawasiliano na wadau wetu na nina furaha kubwa kutangaza namba hizi za simu ambazo wasafiri wanaweza kutumia kuwasiliana nasi kunapotokea jambo lolote linalohatarisha usalama wao.”
“Tumepokea maoni kutoka kwa wasafiri wengi wanaotumia Uber jijini Dar es Salaam, na wameeleza umuhimu wa kupewa namba wanazoweza kutumia kuwasiliana na ofisi zetu kunapokuwa na tukio linalohatarisha usalama wao. Ingawa Uber imeweka kipaumbele kwenye usalama wa wasafiri, tunawashauri wasafiri watumie namba za simu za dharura za kitaifa. Kupitia namba hizi za Timu ya Matukio ya Dharura, tunaweza kuwasadia wasafiri kuwasiliana na Timu yetu ya Matukio ya Dharura haraka iwezekanavyo" ameongeza Bw. Msemo.
Bila shaka ni haki ya kila mtu kujisikia salama, iwe wanatumia usafiri wa treni, taksi, daladala, au anatumia Uber. Ingawa hakuna usafiri ambao ni salama 100% au ambao hauna matukio yanayohatarisha usalama wa msafiri, programu za teknolojia kama Uber zinaweza kusaidia kuimarisha usalama, na ndiyo maana namba hizi za Timu ya Matukio ya Dharura zitakuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha usalama wa wasafiri.
Kutumia namba za Timu ya Matukio ya Dharura (IRT)
● Fungua menyu ya app ya Uber, na ubonyeze 'Usaidizi'
● Bonyeza 'Safari na mapitio ya nauli'
● Chagua safari husika
● Chagua kulikuwa na tukio la kiusalama
● Tuma tiketi ya tukio hilo ukijumuisha namba zako za simu na maelezo mafupi ya tukio husika
● Msafiri atapigiwa simu haraka iwezekanavyo!
Loading...

No comments: