KISHINDO CHA LUGOLA CHATUA KWA KAMISHNA GENERALI WA MAGEREZA, AMFUKUZA KIKAONI

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amemfukuza kikaoni Kamishna Jenerali wa Magereza, Juma Malewa kwa kuchelewa kikaoni.

Lugola amemfukuza Dkt Malewa leo July 6, saa tano asubuhi ikiwa ni dakika chache baada ya kikao hicho kuanza.

Awali, Lugola alisema ikifika saa 5 kamili, mlango ufungwe na kama alivyoagiza, ulifungwa.

Baada ya kuingia Dkt Malewa, Lugola akahoji kwa nini amefunguliwa mlango?
Licha ya Dk Malewa kuomba msamaha, Lugola alikataa kata kata. Pia Lugola ameagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, kumshusha cheo hadi kubaki na nyota tatu, mkuu wa usalama barabarani, Mbeya, Leopold Fungu.

Katika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Ndani ameagiza Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto mkoa wa Kagera, George Mrutu ashushwe cheo.

Kikao hicho ni cha kimkakati cha viongozi wa vyombo na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo.
 Na Amos C Nyanduku

Post a Comment

0 Comments