MAKAMU WA RAIS AFUNGUA NYUMBA 14 ZA NHC MBEYA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, July 30, 2018

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA NYUMBA 14 ZA NHC MBEYAMAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassani amesema ujenzi wa Nyumba za watumishi katika Halmashauri ya Busokelo ni lengo la kupunguza changamoto mbalimbali za wananchi ambapo watumishi hao wanatakiwa kusikiliza shida zao.
Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua Nyumba 14 zilizojengwa na Shirika la Nyumba mkoa wa Mbeya katika Halmashauri hiyo ya Busokelo wilayani Rungwe ikiwa ni pamoja na kupunguza adhaa ya watumishi waliyokuwa wakiipata kutembea kutoka Tukuyu mjini.
Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani Mbeya ni miongoni mwa Halmashauri zilizoanzishwa hivi karibu ambayo kwa asilimia kubwa zimekuwa na changamoto mbalimbali ambazo ni upungufu wa miundombinu.
Shirika la Nyumba Mkoa wa Mbeya limetekeleza mradi wa ujenzi Nyumba za watumishi 14 ilikuweza kukabiliana na changamoto hiyo iliyokuwa ikiwakumba watumishi hao ambapo ujenzi huo umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.1.
Mbunge wa jimbo la Busokelo ameliomba shirika hilo kuweza kuendelee na ujenzi wa Nyumba zingine ilikuweza kupambana na changamoto iliyopo ya upungufu wa Nyumba hizo.
Na Amos C Nyanduku
Loading...

No comments: