RAIS MAGUFULI AAGIZA TANROADS KUTANGAZA TENDA YA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA MSALATO.


Rais Dkt John Magufuli ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wakala wa barabara wa nchini TANROADS pamoja na Wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano kutangaza tenda ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa msalato Mkoani Dodoma  ili kuweza kupokea ndege za kimataifa 
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Julai 30, 2018  akiwa Ikulu jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya kutoa hati za viwanja vilivyopo Dodoma kwa mabalozi 62 wa nchi mbalimbali na mashirika matano ya kimataifa kwa ajili ya kujenga ofisi na makazi. 
Kwa upande wake Waziri wa Ardhi nyumba na mendeleo ya makazi William Lukuvi amesema hati zote zimetolewa bure na serikali ipo tayari kusikiliza maombi ya ziada ya mabalozi.

Na Amos C Nyanduku

Post a Comment

0 Comments