Rais Magufuli Afungua Mkutano Kati Ya Vyama Vya Siasa Vya Afrika Na Chama Cha Kikomunisti Cha China (CPC) Jijini Dar Es Salaam. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, July 17, 2018

Rais Magufuli Afungua Mkutano Kati Ya Vyama Vya Siasa Vya Afrika Na Chama Cha Kikomunisti Cha China (CPC) Jijini Dar Es Salaam.


Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amesema huu ni wakati kwa nchi za Afrika, kuungana pamoja katika mapambano dhidi ya umaskini kwa kuandaa misingi bora ya kiuchumi.
Rais Magufuli amesema hayo leo Juali 17 wakati akifungua mkutano wa kidunia wa vyama vya siasa uliovikutanisha zaidi ya vyama 40 kutoka Afrika na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Miongoni mwa vyama hivyo, saba vilishiriki katika harakati za ukombozi kusini mwa Afrika ikiwamo CCM.

Rais Magufuli amesema kama nchi za Afrika zitashikamana zinaweza kubadili na kukuza uchumi wake.

Pia aliiomba China kusaidia katika ujenzi wa miradi mikubwa inayoendelea nchini ikiwamo ujenzi wa kisasa wa reli ya kati, gesi, mradi wa kufua vyuma wa Mchuchuma na Liganga na uendelezaji wa viwanda.

"Niwaombe China iunge mkono katika utekelezaji wa miradi yetu mikubwa ya kimaendeleo, ushirikiano kiuchumi ndio unaohitajika zaidi," amesema.

Rais Magufuli amesema nchi za Afrika hazihitaji misaada yenye masharti isipokuwa ile ya kirafiki inayojengwa kwenye misingi ya kuelewana.

Awali Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Watu wa China (CPC) Song Tao alisema ili kufikia malengo ya kiuchumi nchi za Afrika zinapaswa kuheshimu haki za binadamu.

Amesema China ipo tayari kusaidia mipango ya kichumi kwa nchi za Afrika na kuwataka wajiandae kulingana na mazingira ya nchi zao.

Amesema japo nchi yao ina watu zaidi ya 2.5 bilioni lakini wameweza kujenga mfumo wa maendeleo na jamii bora yenye manufaa.

Ameshauri vyama vya Afrika kujikita katika kutafuta suluhisho la matatizo ya nchi zao kubwa ikuwa ni kuwaondoa watu kwenye umaskini.
==

Loading...

No comments: